UPANUZI WA MASHAMBA YA KUZALISHA KOROSHO
Kuongeza ukubwa wa mashamba ya Chama ya kuzalisha korosho na mazao mengine ya kibiashara kutoka ekari 82 hadi ekari 300 ifikapo 2030/31.
Kuongeza ukubwa wa mashamba ya Chama ya kuzalisha korosho na mazao mengine ya kibiashara kutoka ekari 82 hadi ekari 300 ifikapo 2030/31.
Kuanzisha kiwanda kimoja cha kuzalisha mafuta ya kula kutokana na mazao ya wakulima, kuongeza thamani ya mazao na mapato ya Chama.
Kujenga maghala makuu mapya mawili katika eneo la Chama ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao ya Wanachama kwa usalama zaidi.
Kuanzisha mradi wa usafirishaji wenye magari kumi na tano (15) kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa za Chama na Wanachama.
Kuanzisha duka la pembejeo za kilimo katika kila Halmashauri ya eneo la Chama (Kilwa, Lindi Manispaa na Mtama) kurahisisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima.
Kujenga ukumbi mmoja wa kisasa kwa ajili ya mikutano na matumizi ya kibiashara, kuongeza vyanzo vya mapato ya Chama.
Mbali na miradi hii, Chama kinatekeleza jumla ya vipaumbele tisa (9) vilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano: Uanachama; Usimamizi wa huduma; Uzalishaji na ubora wa mazao; Masoko na uhusiano na wadau; Usimamizi endelevu wa miradi na uwekezaji; Usimamizi wa fedha na mali; Uongozi, utawala bora na menejimenti ya rasilimali watu; Matumizi endelevu ya TEHAMA; na Utunzaji wa mazingira asilia na kujali jamii.