Bei za Mazao
KOROSHO MNADA WA PILI Bei ya Juu 3290 Bei ya Chini 3030 TZS/kg

Kuhusu Sisi

Ofisi ya Lindi Mwambao

HISTORIA YETU

Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao Ltd kilianza kufanya kazi tarehe 1 Oktoba 2014, baada ya Chama Kikuu cha Ilulu kilichokuwa kikihudumia Mkoa wa Lindi kukoma uhai wake na kuwa chini ya Mfilisi. Kutoka hapo vyama vikuu viwili vipya vilizaliwa — Chama Kikuu cha RUNALI na Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao.

Chama kilipata usajili wa awali (Namba 5596) tarehe 19 Februari 2018, na tarehe 13 Januari 2023 usajili mpya wa kidigitali wenye Namba AFF-LND-LND-MC-2023-24.

Chama kilianza na AMCOS 39 za korosho; hadi sasa jumla ya AMCOS wanachama ni 61, zikitoka katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Lindi — Manispaa ya Lindi, Mtama na Kilwa. Tangu msimu wa 2018/19 wanachama wameongeza uzalishaji wa ufuta na mbaazi, kando na korosho. Makao makuu ya Chama yako Manispaa ya Lindi, Kata ya Rasibula, Mtaa wa Mitwero.

DIRA NA DHIMA

Dira: Kuwa chama cha ushirika kinachoongoza katika kuboresha maisha ya wakulima wa Mkoa wa Lindi kupitia uzalishaji endelevu na masoko bora ya mazao ya kilimo.

Dhima: Kutoa huduma bora za ushirika zenye tija kwa wanachama kupitia uwazi, uwajibikaji na ushirikiano, ili kuongeza kipato na kuboresha maisha ya jamii ya wakulima.

MAADILI YETU

  • Uwazi: Shughuli zote za chama zinafanyika kwa uwazi na uadilifu.
  • Uwajibikaji: Viongozi na watendaji wanawajibika kwa wanachama.
  • Ushirikiano: Chama kinafanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali ili kuboresha huduma.

WASHIRIKA WETU

Chama kikuu cha ushirika Lindi Mwambao Ltd kinashirikiana na Wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanachama wananufaika ipasavyo na shughuli za chama, wakiwemo:
- Copra na Bodi ya Korosho Tanzania
- Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)
- Soko la Bidhaa Mtandaoni (TMX)
- Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE)
- Bodi ya Stakabadhi Ghalani
- Serikali ya Mkoa wa Lindi
- Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (Moshi Co-operative University)
- Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

MUUNDO WA UONGOZI

Chama kinaongozwa na Bodi ya Chama yenye wajumbe saba (7), iliyochaguliwa na wanachama, ikisimamiwa kiutendaji na Meneja Mkuu pamoja na watendaji kumi na sita (16) wa ngazi za juu. Tazama majina ya viongozi wetu hapa chini.

WASILIANA NA UONGOZI

S.L.P 140, Lindi, Tanzania. Simu: +255 685 543 131. Barua pepe: info@lindimwambaoltd.co.tz.

Uongozi Wetu

Bodi ya Chama na Watendaji wa Ngazi za Juu wa Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao (LMCU) Ltd.

Ismail M. Nalinga

Ismail M. Nalinga

Mwenyekiti
Hassan M. Mnumbe

Hassan M. Mnumbe

Makamu Mwenyekiti
Issa A. Baraka

Issa A. Baraka

Mjumbe wa Bodi
Said M. Shahame

Said M. Shahame

Mjumbe wa Bodi
Juma A. Issa

Juma A. Issa

Mjumbe wa Bodi
Hawa A. Mbundu

Hawa A. Mbundu

Mjumbe wa Bodi
Rashidi H. Masudi

Rashidi H. Masudi

Mjumbe wa Bodi
Nurdin S. Swallah

Nurdin S. Swallah

Meneja Mkuu
Lisa E. Mgonja

Lisa E. Mgonja

Mhasibu Mkuu
Bakari S. Saidi

Bakari S. Saidi

Mkaguzi wa Ndani
Hassan S. Dossa

Hassan S. Dossa

Afisa Manunuzi
Glory I. Makere

Glory I. Makere

Afisa Masoko na Uhamasishaji