CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA LINDI MWAMBAO LTD

MIRADI INAYOENDELEA NA ILIYOPANGWA YA LINDI MWAMBAO.
Bei za Mazao
KOROSHO Bei ya Juu 2500 Bei ya Chini 1900 TZS/kg
MBAAZI Bei ya Juu 1500 Bei ya Chini 1000 TZS/kg
UFUTA Bei ya Juu 3500 Bei ya Chini 2500 TZS/kg
Uongozi wa Juu
Ismail M. Nalinga
Ismail M. Nalinga
Mwenyekiti
Nurdin S. Swallah
Nurdin S. Swallah
Meneja Mkuu
Miradi Yetu — Picha
Miradi Yetu
SHAMBA LA KOROSHO

UPANUZI WA MASHAMBA YA KUZALISHA KOROSHO

Kuongeza ukubwa wa mashamba ya Chama ya kuzalisha korosho na mazao mengine ya kibiashara kutoka ekari 82 hadi ekari 300 ifikapo 2030/31.

KIWANDA CHA MAFUTA

KIWANDA CHA KUZALISHA MAFUTA YA KULA

Kuanzisha kiwanda kimoja cha kuzalisha mafuta ya kula kutokana na mazao ya wakulima, kuongeza thamani ya mazao na mapato ya Chama.

MAGHALA MAPYA

UJENZI WA MAGHALA MAPYA YA KUHIFADHI MAZAO

Kujenga maghala makuu mapya mawili katika eneo la Chama ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao ya Wanachama kwa usalama zaidi.

USAFIRISHAJI WA MAZAO

MRADI WA USAFIRISHAJI WA MAZAO NA BIDHAA

Kuanzisha mradi wa usafirishaji wenye magari kumi na tano (15) kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa za Chama na Wanachama.

DUKA ZA PEMBEJEO

MADUKA YA PEMBEJEO ZA KILIMO

Kuanzisha duka la pembejeo za kilimo katika kila Halmashauri ya eneo la Chama (Kilwa, Lindi Manispaa na Mtama) kurahisisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima.

UKUMBI WA MIKUTANO

UJENZI WA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO

Kujenga ukumbi mmoja wa kisasa kwa ajili ya mikutano na matumizi ya kibiashara, kuongeza vyanzo vya mapato ya Chama.

VIPAUMBELE VINGINE VYA MPANGO MKAKATI (2026/27–2030/31)

Mbali na miradi hii, Chama kinatekeleza jumla ya vipaumbele tisa (9) vilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano: Uanachama; Usimamizi wa huduma; Uzalishaji na ubora wa mazao; Masoko na uhusiano na wadau; Usimamizi endelevu wa miradi na uwekezaji; Usimamizi wa fedha na mali; Uongozi, utawala bora na menejimenti ya rasilimali watu; Matumizi endelevu ya TEHAMA; na Utunzaji wa mazingira asilia na kujali jamii.